NILIOLEWA NA WANAUME WANNE
Sehemu Ya (10),
Mwandishi:King B.love,
Instagram:King B.love50.
Ilipoishia:
Baada ya kukutana na kaka aliyeniahidi kunioa,
Alianza kuniuliza Maswali ambayo yalinipatia kigugumizi sana,alianza kuniuliza kazi yangu nayoifanya hapa Mjini,kazi amnayo inaniingizia kipato,
Nilichomjibu nikwamba,"
Mimi ni Mfanyabiashara wa ndani na nje ya Nchi,
Nilijikuta inanibidi kumuongopea tu hakuna namna......................
Endelea:
Kijana wawatu aliamini nilichomwambia, alionyesha kufurahia sana
Kumpata Mwanamke Mfanya Biashara,
Alionyesha yupo Serious kweli kwa kitu anachotaka kukifanya juu yangu.
Alihitaji kujitambulisha kwa Wazazi na Ndugu zangu,ilibidi kumdanganya tena kwamba,
"Mimi sina Wazazi wote walishatangulia mbele ya haki,
Ila nipo na Mjomba Wangu ambae ni
Mdogo wake Marehemu Mama yangu",
Basi kaka huyo alihitaji kujitambulisha ili afate taratibu zote anitolee Posa kwa ajili ya kunioa sasa rasmi niwe Mke halali kwake.
Niliona kama Dhali vile,
Kukutana na kaka mwenye Pesa zake tena
kwaharaka anataka kunioa,
Ilinibidi kumtafuta mtu ili nicheze naye Mchezo,
nimfanye yeye kama Mjomba wangu
Ili kusudi hata Mahali ya Posa apewe yeye,
Ili Mimi niichukue nigawane nae,
Make kiukweli mimi Jijini Dar es alaam,
Nilikuja kutafuta Pesa na sio Mapenzi wala Ndoa.
Basi Mpango wakumtafuta Mjomba feki ulifanikiwa,
Nilimpata kijana mmoja,
Ambae alikua akijihusisha na Mishemishe za hapa na pale Mjini,
Nikampatia Mchongo wakucheza Mchezo kama Mjomba wangu,
Ili yule kaka aweze kutoa Posa juu yangu,
Nilimpanga kwa kila kitu,
Hadi kiasi cha Mali nachokihitaji.
Baada ya kukamilisha Mipango yangu yote,
Nilichukua Simu yangu kwa ajili ya kumpigia sasa kaka Ambae anahitaji kunioa,
Huku nikimuongelea kwa Sauti ya Mahaba na Bshasha tele za Mahabati,
"My Darling!!
Tiyari nimemwambia Mjomba kila kitu kuhusu wewe Honey wangu,
Hivyo yupo kwa ajili ya kukusubilia tu wewe,
Usichelewe tafadhali Mume,
Kwasababu natamani sana kuja kuishi kwangu na Mume wangu,nimechoka kuishi Nyumbani pekee Babe,
Nakutamani sana Mwanaume wangu,please Usiniangushe Mpenzi,"
Nilimvibisha Bichwa kwelikweli Jamaa huyo, Madeko kama yote kumbe anachezewa Kekundu bila mwenyewe kujua.
Alijikuta Anacheka kicheko cha furaha,
Kisha anaongea,"Hahahaaa!
Usijali Mpenzi,mimi niwako tu,
Kwako nimeshakufa nakuoza mazima,
Bado kunizika tu Mrembo,
Umenimaliza kabisaa,
Kwako sijiwezi hata Chembe Sweet Mama wangu"
Nilifurahi Sana kusikia hivyo,
Kwasababu tiyari nilijua Mipango yangu yote imeenda sawa sawia kama nilivyokua nataka.
Kweli jamaa hakuchelewa wala hakupoteza mda hata kidogo,
Kesho yake Ugeni ukafika kwa Mjomba Feki,
Ambae nilimwandaa na kumpanga kwa kila kitu.
Walipofika wakazungumza juu ya Posa,
Mjomba Feki akawapiga kiasi Cha Shilingi Millioni moja Tanzania Shilingi,
Jamaa hakusita kuzitoa
Kwasababu alikua nazo
Tangia Mwanzo, nilimsoma nakugundua Sura yake inaonyesha Pesa ipo,Sura ya Pesa Watoto wa Mjini tunaita hivyo.
Baada ya kutolewa Posa sasa,
Nilimgea Mjomba Feki kiasi cha Shilingi laki Mbili kwa ajili ya Malipo ya kazi yake,Jamaa aliweza kuigiza hatali,
Kama Mjomba wangu kabisa,
Aise hapa Mjini kuna watu ni noma sana,kila mmoja hujitafutia Pesa kwa style yake ndio Maisha ya Mjini.
Nilichukua kiasi cha Pesa nilichokua nimebakiza kama Shilingi laki nane,
Nikaenda kuziweka katika Account yangu,
Ambayo nilikua nimeifungua tangia Mwanzo
Nilipoanza Biashara ya kujiuza Mwili wangu,
Nilipoangalia Salio katika Account yangu hiyo,
Niliikuta inasoma Shilingi Millioni kumi na Mbili Pesa za kitanzania,
nikaamua kutafuta kiwanja Jijini Dar es alaam,
Maeneo ya Zakhiem Mbagala,
Nikanunua kwa Shilingi Millioni nane Pesa za Kitanzania,
Lakini ilikua ni Siri yangu Binafsi,
Sikuweza kumshilikisha yoyote katika Mambo ya Ununuzi wa kiwanja hicho.
Hatimaye kaka huyo alinifanyia Party kidogo,
Kisha nikafunga nae Ndoa nakuanza kuishi nae kabisa akiwa Mumewangu wa kwanza.
Baada ya kua Mke wa Mtu sasa,
Nilishindwa kutulia na Mwanaume mmoja ndani,
Kwani niliamini yeye anajua mimi nimfanya Biashara,
Hivyo atahitaji kuniona nikitoka,
Nilichokifanya sasa,
Niliachana na Biashara ya kujiuza Mabarabarani,
Nikaingia katika Hoteli kubwa sana Jijini Dar es alaam,
Kwa jina naihifadhi kutokana na Usalama wangu Binafsi,
Nikaanza Biashara ya kujiuza(Kudanga)kwa wazungu na watu Mbalimbali wakubwawakubwa,
Ambao walikua wakija Hotelini hapo.
Kilichokua kinafanyika,Mteja akifika Hotelini kama anahitaji Huduma ya Mwanamke,Moja kwa moja alikua akiletwa katika Chumba changu kwa ajili ya kupata Huduma.
Nilikua nikimuanga Mume wangu kwa Bashasha tele
na Mabusu juu,
Akijua naeda nje ya Nchi kufanya Biashara kumbe Mtoto Wakike,
Naingia Hotelini kugawa Mwili wangu kwa Pesa,
Nilikua nakaa huko hata Mwezi mmoja Mzima,
Kisha narudi Nyumbani kwangu.
Basi Mumewangu anakua anafurahi sana mwenyewe akijua Mkewe natoka katika Biashara,
Kumbe nilikua natumika tu na Wanaume tofautitofauti Hotelini,
Kiasi cha Pesa nilichokua nakipata kwa kazi hiyo,
Kilikua kikubwa sana,
Kiasi kwamba kiliniwezesha.continue reading......